Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfungulia mashtaka mapya Salum Njwete
(Scorpion). Mashtaka hayo mapya yanayofanana na yale ya awali ya
unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hata hivyo Njwete amekana shtaka na kurudishwa rumande, huku Hakimu Flora Haule anayesimamia kesi hiyo akizuia dhamana.
Awali Mahakama hiyo ilimfutia mashtaka yanayomkabili Scorpion baada ya
upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu
hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo na Kutokana na maombi hayo, Hakimu
Adelf Sachore alikubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91
kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi
Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi
kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.
Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki upya mshtakiwa huyo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo.
Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi Mrisho.
0 comments:
Post a Comment