Msanii Diamond Platnumz kawatumia ujumbe wasanii wenzake kwenye bongofleva kupitia ukurasa wake wa Instagram ili waweze kufanya vizuri kwenye masoko ya nje.
Tuesday, 2 May 2017
Monday, 24 April 2017
Uteuzi wa Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, unaonekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo.
Wednesday, 19 April 2017
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iko katika mchakato wa kuanzisha “Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa” ambao una dhima kubwa ya kusaidia kuinua kipato, kuongeza tija
Saturday, 8 April 2017
Muda mfupi baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kusema ni lini mwanamuziki Roma na wenzake watapatikana, taarifa kutoka kwa mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana.
Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo imesema imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki” tangu tarehe 5 Aprili 2017.
Wednesday, 29 March 2017
Saa chache baada ya kuachiwa huru kutokana na amri ya Rais John Magufuli, Rapa Nay wa Mitego amesema kuwa atayafanyia kazi maoni ya Rais kuhusu kuboresha wimbo wake kwa namna ya pekee.
Sunday, 26 March 2017
Mwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego (#Trueboy) amekamatwa na Polisi leo asubuhi mkoani Morogoro na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero mkoani humo.
Nay wa Mitego amekamatwa akiwa hotelini Morogoro baada ya kuamaliza shughuli zake zilizompeleka ambapo alitakiwa kuongozana na polisi hao hadi kituo cha polisi.
“Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote. ✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo.” Ameandika Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Licha ya kuwa mwanamuziki huyo hajaeleza sababu ya kukamatwa kwake, au Jeshi la Polisi kutoa taarifa, lakini inaaminika kuwa sababu kubwa ni wimbo wake alioutoa siku za hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wapo.
Wimbo huo umezungumzia mambo mengi hasa ya kisiasa yanayoendelea nchini kwa sasa ikiwa ni pamoja na tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uhuru wa vyombo vya habari na masuala ya sanaa.
Sunday, 19 March 2017
Friday, 17 March 2017
Muigizaji wa Filamu Tanzania Kajala Masanja amewafungukia wanaomsema kwamba ameshindwa kumlea binti yake ‘ Paula’ na kusema anatamani awaoneshe watu hao malezi anayompatia binti yake huyo.
Tuesday, 14 March 2017
Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii wa 'hip hop', Joseph Haule (Profesa Jay) amesema hana kinyongo na wasanii wote waliokwenda jimboni kwake kipindi cha uchaguzi oktoba 25, 2015 kwa ajili ya kumpinga.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempigia simu Diamond Platnumz wakati akihojiwa Jumanne hii kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV.
Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Diamond kwa kupata mtoto wa pili akimueleza kuwa wakati wa kampeni alikuwa na mtoto mmoja.
Naye Diamond hakuchelewa kutupa ombi lake akimtaka Rais kuwasaidia wasanii wa Tanzania.
“Asante sana nimekusikia,” alisema Rais Magufuli. “Lakini nakupongeza sana kwa kuzidi kuitangaza Tanzania katika masuala ya muziki na nawapongeza wanamuziki wote hata wale wanaogiza nawapenda sana wale, Shilawadu nk, asanteni jamani.”
Saturday, 11 March 2017
Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amefunguka kwa kumpa pole mwanadada Vanessa Mdee ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutumia na kusambaza dawa za kulevya.
Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema jeshi hilo bado linawashikilia Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Vanessa Mdee ambaye alikamatwa Jumatano na Rummy Shaeli kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.
Akiongea na wana habari Ijumaa hii ofisini kwake kamanda amesema jeshi hilo bado linawashikilia watu hao mpaka uchunguzi utakapo kamilika.
“Juzi tulimkamata Vanesa Mdee napia tunamshikilia Rummy Shaeli taarifa zinaonyesha ni watumiaji na wasambazaji lakini upelelezi unaendelea na ukikamilika tutawafikisha mahakamani au tutamuachia. Na sio hao tu wapo wengine ambao tuna majina baadhi tumewakamata inasemekana huwa wanasafirisha dawa hizo kwenda Afrika Kusini,” amesema Siro.