Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempigia simu Diamond Platnumz wakati akihojiwa Jumanne hii kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV.
Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Diamond kwa kupata mtoto wa pili akimueleza kuwa wakati wa kampeni alikuwa na mtoto mmoja.
Naye Diamond hakuchelewa kutupa ombi lake akimtaka Rais kuwasaidia wasanii wa Tanzania.
“Asante sana nimekusikia,” alisema Rais Magufuli. “Lakini nakupongeza sana kwa kuzidi kuitangaza Tanzania katika masuala ya muziki na nawapongeza wanamuziki wote hata wale wanaogiza nawapenda sana wale, Shilawadu nk, asanteni jamani.”
0 comments:
Post a Comment