Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi kuhusu kutekwa kwa msanii huyo na wenzake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema kuwa hawezi kusema ni lini wasanii hao watapatikana kwani ni hadi pale upelelezi wanaouendesha utakapokamilika.
Sirro alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyekuwa akiuliza kuhusu lini wasanii watapatikana kufuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa aliyoitoa jana kuwa hadi Jumapili wasanii hao watakuwa wamepatikana.
Haya ni mambo machache aliyoyazungumza:
“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, yamekuwepo na tukafanyakazi tukapata majibu. Tukio hili la kutekwa wasanii ni la kawaida.
“Tukio hili la utekaji ni kama matukio mengine ya uhalifu ambayo tumeyashungulikia, hatuwezi kusema hali mbaya kwa tukio hili.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.
“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu.
“Wanaosema simu ya Roma ilikuwa inapatikana na kuhoji kwanini hatukwenda TCRA, wasitufundishe kazi, wamejuaje hatukwenda TCRA?
“Wengine walalamika wasema leo ni siku ya tatu tumechelewa kutoa majibu walipo, wajue majibu ya polisi kuuawa tulipata baada ya mwezi mmoja.
“Hawa watu hawakuja kuniambia kuwa Kamishna Sirro sasa tunakwenda kuwateka, kwamba ninajua walipo lakini sitaki kuwakamata."
0 comments:
Post a Comment