Friday, 17 March 2017

Kajala amewafungukia wale wanaosema eti ameshindwa kumlea binti yake Paula.|Soma

Muigizaji wa Filamu Tanzania Kajala Masanja amewafungukia wanaomsema kwamba ameshindwa kumlea binti yake ‘ Paula’ na kusema anatamani awaoneshe watu hao malezi anayompatia binti yake huyo.

Akipiga story na eNewz, Kajala amedai kuwa hawezi kushindwa kumlea mtoto wake na kwamba malezi anayompatia binti yake ni tofauti na yale watu wanayoyazungumzia katika mitandao ya kijamii na kuongeza kuwa binti huyo analelewa katika maadili, yanayotakiwa.

“Sijashindwa kumlea mtoto wangu, natamani wangekuwa wanaona malezi ninayompatia Paula kwani kila wanachokiona na kukisikia kwenye mitandao ni tofauti sana na ninavyomlea”. Kajala alisema.

Kajala ameongeza kwamba katika jambo linalomuumiza ni watu kutumia jina la binti yake huyo na kujifanya ni yeye na wakati mwingine kuweka vitu hasi ambavyo vinamfanya mtoto wake achukuliwe tofauti katika jamii.

Aidha muigizaji huyo ameongeza kuwa serikali inapaswa kushughulikia matatizo yanayotolewa na watumiaji wa mitandao kwa umakini wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu ya kutosha.

“Ile akaunti siyo ya Paula kwanza, kwani hajawai kuwa na simu au kumiliki, nimeshawahi kuwaambia wamiliki wa ukurasa huo wabadilishe jina au waandike ni ‘fanpage’ lakini naona wamegoma , Baba yake naye amejaribu kuzifunga lakini bado zinaendelea kutumika mpaka sasa nimechoka ila bado hatujajua tuchukue hatua gani”. Kajala aliongeza.

Paula ambaye ni mtoto wa muigizaji huyo pamoja na Producer P- Funky Majani aliwahi kukutwa na mkasa wa kufananishwa na binti aliyerekodiwa akiwa mtupu na kusambazwa mitandaoni.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top