Ikiwa bado jina la Askofu Gwajima halijafutika vichwani mwa watu kufuatia vita kali ya maneno iliyokuwepo kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, leo Askofu Gwajima kayaandika haya:
“Mungu ni Mungu wa nyakati na majira, hekima kubwa ni kujua cha kutenda wakati wa husika. Hutakiwi kushindana na majira bali fuata majira. Wakati wa baridi huwezi kupambana bila kujifunika na wakati wa joto hutakiwi kupambana nalo bali unatafuta ubaridi. Vivyo hivyo Mungu ana majira yake kwa watu wake. Katika Biblia, wafalme wa zamani walikuwa na watu maalum kwenye jeshi wenye akili Ya kujua nyakati na majira. Tofauti ya tajiri na masikini ipo katika uwezo wa kuziona na kutumia fursa, huwezi kutumia fursa kama hujui nyakati na majira. Ni Maombi yangu Mungu akupe hekima ya kujua nyakati na majira yako. – Bishop Dr Josephat Gwajima
0 comments:
Post a Comment