Tuesday 16 May 2017

Updates: Wakazi wa Jiji la Mwanza wafuriku kushuhudia zoezi la kuung'oa mti wa Maajabu.|Soma

Wakazi wa Jiji la Mwanza leo walifuriku kushuhudia zoezi la kuung'oa mti aina "Mwembe" ambo awali uligoma kutakwa na kung'olewa. 

Mti huo ambao ulikuwa maeneo ya Pasiansi -Iloganza karibu na shule ya Msingi Isenga ulikuwa ukihusishwa na imani za kishirikina kutoka na majaribio mbalimbli kushindwa kuukata ama kuung'oa mti huo wa mwembe pamoja na kusababisha uharibifu wa Caterpiller iliyojaribu kuusukuma mwembe huo na dereva wake kukimbia kusikojulikana. 


Mara tu baada ya kung'olewa watu walivamia eneo ulipokuwa kuwa mti huo wa Mwembe na kuanza kuchukua mizizi ya mti huo.

Pia kwa taarifa zisizo rasmi inasemekana kuwa watu wote ambao awali walijaribu kuukata ama kuung'oa mwembe huo wapo hoi na wamelazwa hospitalini. 





0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top