Zoezi la Uhakikiki wa watumishi wa umma limeanza Nyamagana
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA, imezinduaa zoezi la usajili wa watumishi
wa umma katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza katika Shule ya
Sekondari Mwanza , linalolenga kubaini na kutatua tatizo la watumishi
hewa.
Zoezi
hilo limezinduliwa na mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary Tesha Onesmo
katika Shule ya Sekondari Mwanza kwa kuwahimiza watumishi wote wa umma
kujitokeza na kusajiliwa kwa wakati ili zoezi hilo kukamilika kwa wakati
uliopangwa ambapo litafanyika kwa muda wa wiki mbili na kumalizika
Oktoba 17, 2016.
0 comments:
Post a Comment