MWIGULU: Taarifa rasmi za tukio la kupigwa Mwanafunzi.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba leo ametoa taarifa rasmi juu ya tukio la mwanafunzi kupigwa na walimu huko mbeya kupitia ukurasa wake wa facebook ameeleza;
"Taarifa rasmi za tukio la kupigwa Mwanafunzi
Mnamo Tarehe
28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day
sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa,
John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.
Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi
hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi
kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu
wakamchukua na kumpeleka staff room na
kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana
shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni
mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka
kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya
Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka
hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao
walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo". MWIGULU Nchemba,
W MNN
0 comments:
Post a Comment