Meya wa Ubungo kufungua kesi ya jinai dhidi ya RC Makonda kwa kuwa na vyeti feki.|Soma
Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki.
Jacob pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora.
Jacob ameeleza kuwa kesi hiyo itasimamiwa na mawakili maarufu Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Peter Kibatala..
Kesi hiyo itafunguliwa wiki ijayo baada mawakili hao kumaliza mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Machi 18 mwaka huu ambapo Tundu Lissu ni mmoja wa wagombea wa kiti cha urais
0 comments:
Post a Comment