Magufuli atoa siku 60 Tanesco kupeleka umeme kwa Bakhresa
Rais John Pombe Magufuli ametoa siku 60 yaani miezi miwili kwa shirika la umeme nchini (Tanesco) kupeleka umeme wa megawati 10 katika kiwanda cha vinywaji baridi cha Bakhresa huko Mukuranga, Pwani.
Rais amesikitishwa na kitendo hicho cha shirika la umeme nchini (Tanesco) kushindwa kuchanganukia fursa hasa katika viwanda ambao ndio wateja wao wakubwa. "Nashindwa kuelewa hivi hawa Tanesco watawezaje kufanya biashara kama hawataki kuwafikia wao. Nataka kufikia Disemba mwaka huu umeme uwe umefika hapa" .
Aitaka Tanesco kutambua kipaumbele cha taifa ambacho ni kuwa na uchumi wa viwanda. Amesema viwanda vinahitaji umeme wa kutosha kwa sababu vinasaidia katika kuzalisha ajira kwa watanzania.
0 comments:
Post a Comment