Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, akanusha taarifa za kutenguliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
Kwenye mitandao ya kijamii leo October 19,2016 imesambaa taarifa kuhusu Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Kufuatia taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa
amekanusha taarifa hiyo akieleza kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli
imetengenezwa na waharifu hivyo amewataka wananchi kuipuuza.
0 comments:
Post a Comment