Wednesday 12 October 2016

Samsung wamewataka wateja wao kutupa ‘Galaxy Note 7’, zina tatizo la kulipuka kwenye chaji,

Kampuni ya Samsung imetoa tamko rasmi kupitia tovuti yake ikiwataka watumiaji wa simu hizo toleo la ‘Galaxy Note 7’ duniani kote kuchukua tahadhari na kuacha kabisa kuzitumia  wakati ikiendelea na uchunguzi zaidi.
 
Tamko hilo linatokana na kuwepo kwa ripoti za matukio mengi ya watumiaji wa simu za Samsung kulipukiwa na simu hizo wakati wa kuchaji, kampuni hiyo ya Kikorea hatimaye imewataka watumiaje wake kutupa toleo la ‘Galaxy Note 7’ kutokana na tatizo hilo. 

 

“Tunafanya kazi na Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusu kuwepo kwa ripoti za matukio yanayohusu Galaxy Note7. Kwa sabababu usalama wa mteja wetu ni kipaumbele, Samsung tunawataka wauzaji wote wa simu zetu duniani kuacha mara moja kuuza Galaxy Note 7,” Wamesema Samsung.


0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top