Hillary Clinton amehudumu katika nyadhifa nyingi siasa za Marekani, alikuwa mama wa taifa, seneta, waziri wa mambo ya nje. Sasa, anajaribu kwa mara ya pili kutimiza ndoto yake kuu, kuwa rais wa Marekani.
Mwanasiasa huyu wa Democtratic wa umri wa miaka 68 alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Rais Barack Obama mwanzoni mwa utawala wake Januari 2009.
Alijiuzulu muda mfupi baada ya Rais Obama kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.
Ni mwanadiplomasia mashuhuri Marekani na anafahamika sana kwa kusafiri sana nchi mbalimbali na kufuata diplomasia ya kukutana ana kwa ana na wahusika.
Kuzoea kwake kufanya safari nyingi za kuchosha, kunamuandaa vyema kwa changamoto za safari nyingi za kampeni za urais.
Alijaribu mara ya kwanza kuwania urais lakini akashindwa na Rais Obama wakati wa mchujo wa chama cha Democratic mwaka 2008.
Hillary Rodham Clinton
Alizaliwa 26 Oktoba, 1947 mjini Chicago
Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Sheria cha Yale, 1973
Aliolewa na Bill Clinton mwaka 1975
1993-2001: Alipigania kupanuliwa kwa bima ya afya na haki za wanawake alipokuwa mama wa taifa
Alichaguliwa seneta wa New York mwaka 2000
Alichaguliwa tena kwa kura nyingi 2006
2008: Alishindwa mchujo wa kuteua mgombea urais chama cha Democratic
2009-2013: Alihudumu kama Waziri wa mambo ya nje
Chanzo cha Habari: BBC
0 comments:
Post a Comment