Rais Magufuli: Atema cheche ugomvi wa Lema na Gambo kwenye uzinduzi wa mradi.
Rais John Pombe Magufuli amesema hapendi kuona mtu yeyote akimchelewesha kutekeleza ahadi zake za kuwaletea wananchi maendeleo, na wananchi wa Arusha watakuwa wakitafakari kauli hiyo baada ya kushuhudia siasa zikivuruga uzinduzi wa mradi wa maendeleo wa Sh9 bilioni.
Mradi huo ni ujenzi wa hospitali ambayo inalenga kuhudumia bure kina mama na watoto, na ambao sehemu kubwa ya gharama zake imeahidiwa na wafadhili kutoka Marekani.
Tukio la jana. ambalo lilitokea mbele ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo na wafadhili wa ujenzi huo ambao ni taasisi ya Martenity Africa, lilitokana na Gambo kutoa historia ya mradi huo, akimtaja wakili Nyanga Mawalla kuwa ndiye aliyetoa eneo kwa ajili ya ujenzi huo, Jambo ambalo Lema alilipinga akisema mteule huyo wa Rais anapotosha ukweli.
0 comments:
Post a Comment