Tuesday 18 October 2016

Bomu la jeruhi Askari Polisi na raia wanne.

Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kogoma.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, akielezea tukio hilo alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14. Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda (49) mkazi wa kijiji hicho. Pia aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hasna Nasibu, wote wakazi wa kijiji cha uvinza.


Alisema askari walipata taarifa kutoka kwa raia raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza Madukani alikokwenda kununua mahitaji. Alidai kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa asiuawe kwa kipigo.


Mtui alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema alificha bunduki kijijini kwao Lukole wilayani Ngara mkoani ambako askari walikamata bunduki aina ya SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa ardhini. Pia walikamata magazini saba, moja ilikuwa na risasi 40, nne (risasi 30 kila moja) na risasi 75 zilikuwa kwenye mfuko wa sandarusi. Pingu moja na funguo zake, maski tisa na laini 20 za mtandao wa Halotel ambazo hazijasajiliwa.


Mtui alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia juzi akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni). Alisema majeruhi wote watano walipata matibabu hospitalini hapo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

 

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top