Tuesday, 18 October 2016

Mbunge apokea mishahara mitano ya utumishi hewa

Profesa Norman Sigalla ameingia kwenye headline za Sakata la watumishi hewa, Profesa Sigalla ambaye ni Mbunge wa Makete kupitia (CCM), Pia alikuwa mkuu wa wilaya ya Songea.


Profesa Sigalla anadaiwa kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi mitano baada ya kuacha kazi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu na baadae kuchaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya CCM. Hali hiyo imeisababishia serikali hasara ya sh23 milioni.


Baada ya kuacha kazi hiyo ya kuteuliwa na Rais, inadaiwa kuwa Profesa Sigalla aliendelea kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa sh4.6 milioni kutokana na ofisa utumishi wa ofisi wa Ruvuma kumrudisha kwenye oridha ya malipo ya mshahara. Profesa huyo alikuwa ameshafutwa kwenye orodha hiyo tangu Septemba 4 mwaka jana.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top