Samia: Tunatumia sh900 bilioni kwa mwezi kulipa madeni.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hasan amesema Serikali inatumia Sh900 bilioni kati ya Sh1.33 trilioni inazokusanya kila mwezi, kulipa madeni. Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya nchini mjini Dodoma jana.
Kauli yake imekuja wakati kukiwa na mjadala kuhusu uchumi, baadhi ya watu wakisema hali inazidi kuwa mbaya wakati taasisi za Serikali zikitoa takwimu zinazoonyesha kuwa uchumi uko imara. Alisema takriban robo tatu ya fedha zinazokusanywa zinatumika kulipa madeni.
"Kwa bahati mbaya wakati sisi (Serkali ya Awamu ya Tano) tulipoingia tulikuta tayari umeshafikia muda wa kulipa madeni," alisema.
Alisema fedha hizo, theluthi moja ya mahusanyo hayo huenda kwenye malipo ya mishahara ya watumishi wa umma. Aliwataka viongozi hao kusimamia makusanyo na matumizi kwa uhakikisha kuwa mashine za elektroniki zinafungwa katika hospitali nchini.
Alizungumzia pia tatizo la upatikanaji wa dawa akisema Serikali inafikiria kuanziasha mfuko endelevu ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana. Aliwataka madaktari hao kusema iwapo kuna upungufu wa dawa amabyo hutumika kwa wajawazito wanaojifungua ili kuzuia utokwaji wa damu nyingi kwa kuwa muda wa siku mbili, amefanya uchunguzi wake na kubaini wanaojifungua wa mekuwa hawachomwi sindano ya kudhibiti damu.
"Hili sasa halifanyiki na kama linafanyika linaangalia huyu ni nani au katoa nini. Hii ni kuokoa maisha ya kina mama. Kama hazipo mtuambie tuhangaike kuzitafuta ili tuokoe maisha ya wanawake," alisema.
0 comments:
Post a Comment