Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja
Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni
utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye
ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili
haliko kwenye vyeti.
Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea
zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni
Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi
nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto
wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua
kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja
Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama
akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa
jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi
mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna
wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa,
majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.
Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka
yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza
1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili.
Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze
kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe
shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye
kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani
tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu
mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa
nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu
mwenyewe.
Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.
Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu
na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea
baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au
amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu.
Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na
wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa
John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga,
la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.
Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia,
na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la
serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.
Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine
aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na
nyakati na mazingira
Mwigulu,
0 comments:
Post a Comment