Saturday 11 March 2017

Lema kwa mara ya kwanza amefanya mkutano baada ya kutoka Gerezani.|Soma

Na, Vero Ignatus ,Arusha:

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoka rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne.

Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamilisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia, sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.

Amewataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top