Monday 13 February 2017

Dkt. Slaa amulilia Gwajima baada ya kuhusishwa na "Sakata" la Dawa za Kulevya.|Soma

Dk.Wilbroad Slaa

Vita ya kupambana na dawa za kulevya nchini iliyopamba moto zaidi na kuzua mijadala tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipoanza kutaja majina ya watuhumiwa imemuibua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa.

 

Dkt. Slaa ameibuka baada ya kutajwa na kuhojiwa kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye alikuwa rafiki yake na ‘muwezeshaji’ wake kabla siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hazijawageuza kuwa mahasimu. 

 

Akizungumza jana kanisani kwake wakati akiwasimulia waumini wake mkasa uliompata tangu alipowasili katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam hadi alipoachiwa, Askofu Gwajima alisema kuwa alipokea ujumbe wa Dk. Slaa ambaye alimtetea dhidi ya tuhuma hizo. 

 

Ujumbe wenyewe umewekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Askofu Gwajima na unasomeka hivi hapa chini.

 

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top