Friday 17 March 2017

Tundu Lissu afikishwa mahakamani nakusomewa mashitaka Matano (5) na kuachiwa kwa dhamana.|Soma

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Mbunge Tundu Lissu aliyefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matano.

Lissu amesomewa Mashitaka matano(5) ambayo ni yale yale aliyofutiwa hapo awali kuhusu maneno ya Uchochezi kwenye Uchaguzi wa Dimani,Zanzibar.

Serikali imesema upelelezi umekamilika na ikaomba kesi ianze kusikilizwa leo. Lissu aliiomba mahakama isisikilize kesi hii leo ili akashiriki Uchaguzi wa TLS utakaofanyika kesho mkoani Arusha.

Mahakama imekubali maombi ya Tundu Lissu na kumwachia huru kwa dhamana ya milioni 10 ambapo tayari amekwishapanda ndege kuelekea jijini Arusha Kushiriki Uchaguzi huo

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top