Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Dkt John Pombe Magufuli juzi akiwa yupo mkoani Dodoma, alipata nafasi ya kufanya kikao na wabunge wa chama hicho ambapo alizungumza mambo mbalimbali ambayo hafurahishwi nayo kama kiongozi mkuu wa chama.
Rais Magufuli alikutana na wabunge hao katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumza nao ni pamoja na kuwaambia kuwa anafahamu baadhi ya wabunge wanampinga Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
"Nafahamu baadhi yenu mnampinga Waziri Mkuu na mnataka aondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye, naomba niwaambie kuwa hamtafanikiwa. Mimi namuunga mkono msaidizi wangu huyuo kwa asilimia 100 kwa nimejionea mwenye namna anavyoweza kufanya kazi, "alisema Rais Dkt Magufuli na kuongeza.
"Hata mkimuondoa, nikija kuteua mwingine nitamleta huyu huyu na endapo mtamkataa basi nitavunja bunge wote mrudi kwenye uchaguzi."
0 comments:
Post a Comment