Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda Jana Machi 15, 2017 ametimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Machi 13, 2016 na kuapishwa Machi 15, 2016.
Hizi ni baadhi ya nukuu zake:
1.Namshukuru Rais Magufuli kwa kusikiliza kauli ya Mungu na kunikabidhi mamlaka ktk mkoa huu wa Dar.
2.Navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kuwa daraja kati ya Serikali ya Mkoa na wananchi. Wamefanya kazi kubwa!
3.Nawashukuru sana vijana tuliowakamata wa mwanzo(TID na wenzake), wamekuwa mfano mzuri kwa wenzao na Mungu awasaidie
4.Mwaka wangu wa II nikiwa kama RC wa Dar, kasi itaongezeka maana nimekomaa sasa. Nitahakikisha jiji linarudi kwny mstari.
5.Kuna makampuni ya barabara mawili nimeshayapiga marufuku kwa sababu ya kujenga barabara chini ya viwango.
6.Katika vitu nimeweka msingi mzuri ni kinondoni, kesi za ardhi zinasikilizwa mpaka jumamosi
7.Kazi hii nimepewa na Mungu, acha idadi ya wanaomchukia Makonda waongezeka lakini niwe na uhakika na Mungu wangu
8.Tumeamua kufanya vitu hadharani kwa sababu hatutaki kupokea rushwa wala fedha haramu
9.Hatuna kisasi na mtu, ndio maana upande huo wanapigana sisi tunacheka
10.Kupitia fedha za dawa za kulevya, watu wamejenga maghorofa yanakwenda kwa kasi sana na wamefanya hata thamani ya viwanja ipande
11.Fedha hizi za dawa za kulevya zinaenda kukauka DSM ili kila mtu ale kwa jasho lake
12.Tutaanza mfumo wa kutumia kadi ili tukusanye kodi yetu na kila mtu ale kwa jasho lake, kuna watu wanaficha fedha
13.Kipindi hiki ni cha kazi. Nawapongeza wote wanaofanya kazi kwa bidii na kuifanya Serikali isimame kidete
0 comments:
Post a Comment