Monday, 15 May 2017

Picha: Mti wa Maajabu wadaiwa kukwamisha shughuli za upanuaji wa barabara Mwanza.|Zitazame

Kufuatia kuendelea kwa shughuli za upanuaji wa barabara ya Airport Jijini Mwanza, watu wamefurika, magari na pikipiki kusimama barabarani kushuhudia mti aina ya "Mwembe" unaosadikika kuwa ni wa maajabu unaodaiwa kuongea, kutoa machozi ya damu na kushindwa kuanguka mara baada ya kukatwa katika eneo la Isenga Shule ya Msingi. 

Sitofahamu hiyo imeanza kusikika toka juzi baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa majaribio mbalimbali ya kujaribu kuukata "Mwembe" huo kushindwa, awali inasemekana kuwa Jeshi la Magareza la Butimba kupitia wafungwa wake kushindwa kuukata mwembe huo kwa maadai ya kuwa wakiukata unalia na kutoa machozi ya damu, aidha jaribio lingine lilifanyika la kuukata mwenbe huo kwa kutumia "Chain Saw" lakini pia ilishindikana baada ya kuukata mwebe huo na kushindwa kuanguaka na jitihada zaidi kuongezwa kwa kuleta Caterpillar kujaribu kuusukuma mwembe huo ili uanguke kushindwa pia na kusababisha Caterpillar hilo kuharibika pale.


Kufuatia taharuki hiyo chombo chetu kilifanya jitihada za kupata ukweli wa taarifa hiyo kutoka kwa wafanyakazi wa eneo hilo ili kudhibitisha ukweli wa taarifa hizo na kubahatika kukutana na mmoja wa wafanyakazi wa eneo hilo 'Kibarua'  ambae jina lake halikufahamika mara moja na kukanusha taarifa hizo kwa kusema:

"Kaka hapa hakuna kitu na tumeshasema sana hamna kitu lakini kwa kuwa sisi watu weusi ni wagumu kuelewa basi acha watu wajae hapa lakini hamna kitu na huu mwembe utaondelewa hapo mara baada ya taratibu kukamilika".


0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top