Friday 12 May 2017

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaifutia leseni na kuifunga benki nyingine.|Soma

Benki Kuu ya Tanzania imeifungia Mbinga Community Bank PLC, kusitisha shughuli zake zote za kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenk kuanzia leo Alhamisi 12 mei,2017 huku sababu ikitajwa ni ukata uliyoikumba benki hiyo.

Uamuzi wa kuifungia benk hiyo umekuja baada ya Benki kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank ina upungufu mkubwa wa mtaji na Ukwasi kinyume cha matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha za mwaka 2006 na kanunui zake.

“Upungufu huu wa mtaji na ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kuna hatarisha usalama wa amana za wateja “– Taarifa kutoka BoT ilieleza.

Taarifa kutoka Benk kuu ya Tanzania imedai kuwa pamoja na kuifungia benk hiyo tayari imekwisha iweka MbingaBank chini ya bodi ya ufilisi na kuteua bodi ya bima ya Amana kama mfilisi kuanzia leo tarehe 12 .

Aidha, Benki Kuu imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”

Benki Kuu ya Tanzania imewataka wenye amana, wadai na wadaiwa wa iliyokuwa Mbinga Community Bank kuwa wavumilivu kwa Mfilisi, wakati muafaka atawafahamisha wenye amana, wadai na wadaiwa utaratibu wa malipo wa madai, ulipaji wa madeni na taratibu nyingine zitakazohitajika kwa mujibu wa sheria.

Benki Kuu ya Tanzania imechukua uamuzi wa kuifunga benki hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 56(1) (g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2) (i), 11(3) (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top