Wednesday 29 March 2017

Majina ya wanachama 12 walioteuliwa kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia CCM|.Soma

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza majina ya wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye mkutano wa Bunge ujao.

Akisoma majina hayo leo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa wameteua wananchama hao miongoni mwa wengi zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu kugombea nafasi hizo.

Mchanganuo

Miongoni mwa wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6 watatoka CCM. Kufuatia idadi, hiyo CCM imesema kuwa itatoa wabunge watatu wa kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne watatokea Tanzania Bara na wawili watatokea Tanzania Visiwani.

Walioteuliwa kugombea nafasi hizo ni;

Wanawake Tanzania Bara:

1. Zainabu Rashid Mafaume Kawawa

2. Happiness Elias Lugiko

3. Fancy Haji Nkuhi

4. Happiness Ngoti Mgalula

Wanaume Tanzania Bara:

1. Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe

2. Adam Omari Kimbisa

3. Anamringi Issay Macha

4. Charles Makongoro Nyerere

Wanawake Zanzibar:

1. Maryam Ussi Yahya

2. Rabia Abdallah Hamid

Wanaume Zanzibar:

1. Abdallah Hasnu Makame

2. Mohammed Yussuf Nuh

Miongoni wa wagombea hawa 12, Bunge litapiga kura kuchagua wabunge sita watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top