Thursday 6 April 2017

Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza Jeshi la Polisi kumkamata Mbunge Halima Mdee.|Soma

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.

Pia Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi huo wa EALA.

Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo na anatakiwa kufika leo.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top