Monday, 10 April 2017

Hussein Bashe atumiwa ujumbe kuwa ni katika ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya.|Soma

Mbunge wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo.

Bashe ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter na Instagram kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka;

“Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.

"Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la Haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. "

Kufuatia vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu wasiojulikana.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top