Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa siku 14 kwa Shirika la Visiwani Zanzibar (ZECO) kulipa deni lote la ankara za umeme wanalodaiwa na endapo halitafanya hivyo basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kukatiwa umeme.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt. Tito Mwinuka alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2017, Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) lilikuwa linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 127.8.
“Shirika la umeme linashindwa kutekeleza majukumu yake mbalimbali kwa wakati ikiwemo uendeshaji wa shirika, matengenezo ya miundombinu pamoja na utekelezaji wa miradi, hayo yote yanasababishwa na malimbikizo ya madeni kwa wadaiwa sugu hivyo tunatoa siku 14, wasipoweza kulipa tutawakatia huduma ya umeme”. Alisema Dkt Mwinuka
0 comments:
Post a Comment