Saturday 22 October 2016

Watoto wa mitaani wahanga wa ukatilii

UTAFITI uliofanyika na Shirika la Kimataifa la Railway Children Africa (RCA) umesema kuwa asilimia 100 ya watoto wa mitaani wamewahi ama kunyanyaswa kimwili au kwa maneno. Utafiti huo umesema kwa kipindi cha miaka mitatu watoto wa mitaani wenye umri chini ya miaka 14 wamepungua kwa asilimia 40 jijini Mwanza.

 

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana juu ya matokeo ya utafiti huo Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa shirika hilo, Peter Kent alisema, pamoja na kupungua kwa watoto wa mitaani bado watoto hao wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia. Kent alisema kuwa katika jiji la Mwanza linaonyesha asilimia 100 ya watoto wasichana na asilimia 25 ya wavulana wamedhalilishwa kijinsia. 

 

"Watoto na familia zinazoathiriwa na ukatili mara nyingi hutengwa na kuna uwezekano wa kutonufaika na mipango endelevu na badala yake wanahitaji huduma zaidi za kiushauri ili kutibu majereha yaliyotokana na ukatili katika familia zao," Alisema

 

Alisema utafiti huo pia umeonesha watoto wanaokumbwa na vitendo vya ukatili katika umri mdogo mara nyingi husababisha mzunguko wa umaskini na kuwa katika hatari zaidi na matokeo hasi ya maisha.

 

Naye Ofisa Miradi wa Shirika hilo Adamu Kaombwe alisema, kutokana na sababu mbalimbali walizozipata katika utafiti huo wameamua kuandaa kongamano maalum ili kuwakutanisha wadau mbalimbali na kujadili namna ya kutatua.

 

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top