Saturday, 22 October 2016

Mwanza: Mkurugenzi aliyemdekisha Mwalimu kukiona cha Moto

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliud Mwaiteleke, aliyemdhalilisha Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Shilala, Hamis Sengo, kwa kumwamuru kudeki darasa zima mbele ya wanafunzi wake, Wizara ya Tawala za Serikali na mikoa inashughulikia suala hilo.

 

Naibu waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, alisema wamepata taarifa kuhusiana na tukio hilo na watawasiliana na Serikali ya Mkoa wa Mwanza kujua kilichotokea. Alisema awali wanataka kujua hatua zilichukuliwa na uongozi wa mkoa ndipo watajua taratibu stahiki za kuchukua kwa Mkurugenzi huyo.

 

"Tumepata taarifa kuhusiana na tukio hilo la Mkurugenzi wa Misungwi tunafanya sasa kama Wizara ni kuwasiliana na uongozi wa mkoa watueleze kilichotokea na baada ya hapo waseme wamefanya nini tutaanzia hapo walipofika,'' Alisema Jafo.

 

Inaelezwa kuwa Mkurugenzi huyo alifika shuleni hapo, akiwa na watendaji wengine wa wilaya na kukuta madarasa machafu, ndipo alimuamuru mwalimu huyo kudeki darasa zima mbele ya wanafunzi wake, jambo ambalo limepingwa vikali na kulaaniwa na Chama cha Walimu (CWT), wilayani humo.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top