Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha serikali ya awamu ya tano inatimiza azima ya sera yake ya serikali ya viwanda, jana
tarehe 07 Oktoba, 2016 amekutana na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania
katika nchi mbalimbali duniani ambapo aliwataka watilie mkazo katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda.
Mkutano huo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa, Rais Magufuli aliyehutubia na kuongoza majadiliano juu ya
masuala mbalimbali ya shughuli za mabalozi, alisema Tanzania imeweka
dhamira ya kuikuza sekta ya viwanda kutoka ukuaji wa asilimia 7.3 hadi
kufikia asilimia 15 ifikapo mwaka 2021 na kuzalisha ajira kwa asilimia
40.
“Sasa
nimeona niwaite waheshimiwa Mabalozi ili tuelewane, mjue mwelekeo
tunaoutaka na mjue ni namna gani mtakavyoshiriki kuhamasisha uwekezaji
wa viwanda. Nataka
badala ya kubaki mmejifungia ofisini, mtoke mwende mkawatafute
wawekezaji waje wawekeze katika viwanda ili nchi yetu inufaike kwa watu
wetu kupata ajira, Serikali kukusanya kodi na tuinue maendeleo yetu” alisema Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment