Wednesday 12 April 2017

Waziri Mwakyembe atoa sababu za kuwepo kwenye mkutano wa waandishi na Roma.|Soma

Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, Jumanne hii alipata nafasi ya kusimama bungeni Dodoma ambapo alielezea kushangazwa na kitendo cha Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kuwepo kwenye mkutano wa waandishi wa habari na rapper Roma aliyetekwa hivi karibuni na watu wasiojulikana.


Hatimaye Dkt Mwakyembe, Jumatano hii amesimama bungeni kujibu hoja hiyo:


“Nianze na suala la kwanza ambalo ni la uelewa ambalo mheshimiwa Nkamia alionyesha mshangao hapa kuniona mimi niko na msanii Roma Mkatoliki anayedaiwa kutekwa na wenzie watatu siku chache zilizopita. Mheshimiwa mwenyekiti wakati namsikiliza Nkamia jijini Dar es Salaam nilikuwa na kundi kubwa la waandishi wa habari na wao walikuwa wanamshangaa kwanini anashangaa nikiwa kiongozi kwenye idara hii anaelewa kuwa idara ya habari maelezo ni wizara ya habari,utamaduni, sanaa na michezo, kwahiyo ni ofisi yangu ile, na hivi karibuni tumehamia Dodoma Makao makuu yapo pale LAPF. Nikiwa Dar es Salaam ofisi yangu ipo Maelezo kwahiyo mtu akinikuta maelezo mimi ndiyo nimemfuata yeye au yeye ndiyo kanifuata? Sasa ni vitu ambavyo vinatakiwa vieleweke,” alifafanua.


“Mheshimiwa mwenyekiti kijana huyo alipokuwa amepotea mimi ndiyo nilikuwa napigiwa simu na ndugu zake na waandishi wa habari, hakupigiwa Nkamia na mtu mwingine, napigiwa mimi, mimi ndiyo mlezi wa hii sekta na mimi nilikuwa nahangaika na polisi huyu kijana kaenda wapi! Ni vitu ambavyo katika taifa hili hatujavizoea sasa huyu kijana anakuja kuniona ofisini kwangu kimekuwa kioja tena? Amekuja nimekuwa na mkutano naye for one hour ofisini kwangu lakini yule kijana ana picha tofauti na ramli zinazopigwa huko nje na humu ndani ndani ya bunge.”


“Amesema Mheshimiwa naomba aliyeniteka uchunguzi ufanyike in detail kuwa na bastola haina maana mtu atoke serikalini, bastola kila mtu anazo, alichoomba alisema tafadhali naomba uchunguzi ufanyike kwa kina mimi niliona lazima nimsindikize ni suala ambalo ni topical nchini I am the minister responsible ili kuhakikisha kwamba Watanzania wanaacha kupiga ramli, tunapata ushahidi wa kutosha ndiyo upepelezi,” alisisitiza. 

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top