Rais Magufuli leo kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya kisasa (Standard Gauge).|Soma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli leo anatarajia kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya kisasa (Standard Gauge) katika eneo la Pugu Jijini Dar es salaam.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alipotembelea eneo la mradi huo lililopo Pugu Jijini Dar es salaam. Alisema kuwa mradi huo utazalisha ajira nyingi katika kada mbalimbali.
Aidha, aliongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utarahisisha usafiri wa kutoka Dar es salaam hadi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Mwanza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa kuwa safari ya Dar es salaam hadi Morogoro itatumia muda wa saa 1:16, huku Dar es salaam hadi Dodoma itatumia masaa 2:30 na safari ya Dar es salaam hadi Mwanza itatumia masaa 7:30.
Mradi huo ambao uko chini ya Kampuni za Merkezi ya Uturuki na Mota-Engil Afrika ya Ureno, kwa awamu ya kwanza utaanza na kipande cha kilomita 300 kati ya Dar es salaam hadi Morogoro kwa gharama za dola bilioni moja za Marekani.
0 comments:
Post a Comment