Tuesday 7 March 2017

Wanafunzi wa Sekondari Bariadi wa kiona cha Moto baada ya kuandamana na kufunga barabara.|Soma

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo katika halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga barabara kuu ya Bariadi –Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Deus Toga. Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri,lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi la polisi kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo. 

 


Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabara hiyo waliamua kuandamana tena kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana pia baada ya askari hao kuwazuia tena eneo la Hospitali teule ya mkoa (Somanda). Baada ya hali hiyo wanafunzi hao ambao ni kidato cha kwanza hadi cha sita waliamua kukaa katikati ya barabara huku wakiimbanyimbo za kushinikiza kuwa hawamtaki mwalimu Paul Lutema ambaye alikuwa amepelekwa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.

 


“Hatumtaki mwalimu Lutema……tunamtaka mwalimu wetu Toga…..hatumtaki Lutema……Tunamtaka mwalimu Toga”

 

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top