Wednesday 8 March 2017

Makonda: Kupitia siku ya Wanawake duniani ameendelea kupiga vita Dawa za kulevya.|Soma

Mhe. Paul Makonda

Kupitia ukurasa wake wa Instaram Makonda ameandika haya

“Asilimia kubwa ya WANAWAKE ni aina ya watu waliokuza watoto wao katika mazingira magumu, mateso, machungu na kunyanyasika kwa hali ya juu mara nyingine, na walikubali kupitia hayo ili tu MTOTO ASIMAME na kuwa mtu atakaejitegemea na kutegemewa siku moja, LAKINI kuna kundi kubwa lililodhamiria kwa makusudi kabisa kuwarudisha nyuma kwenye mategemeo yao hayo, kundi lililopanga kwa makusudi kabisa kuangamiza vijana wao kwa ajili ya maslahi yao binafsi, kundi lisilojali kwa namna yoyote struggle za kina MAMA hawa katika kuwakuza watoto wao, kundi linalowaharibu huku wakiwa WANAJUA kabisa athari kwa TAMAA TU ya mali za haraka. Kundi la WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA.

Siku ya leo tunapoadhimisha SIKU YA WANAWAKE DUNIANI napenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia kina MAMA wote na wananchi wa mkoa wangu wa DAR ES SALAAM kuwa sitakubali watoto mliowabeba matumboni mwenu miezi tisa na kuwalea kwa tabu wafe kwa MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA. Naomba tuungane na Muheshimiwa Rais wetu Magufuli kuhakikisha tunashinda dhudi ya wauaji na wanyinyaji wanaofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya. Kama uliweza kumtunza tumboni miezi tisa basi usikubali mtoto wa mwingine akakarisha matumaini yako, mlinde mwanao ili ule matunda ya uzao wako..”

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top