Saturday, 11 March 2017

Kesi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake sasa kusubiri ushahidi kutoka nje ya nchi.|Soma


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.

Hayo yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

Baada ya taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na siyo kuleta lugha za ujanja ujanja.

“Tunaomba upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la kutueleza umekamilika ndani ya nchi lakini nje bado, haileti maana yoyote.”Amesema Magafu.

Akijibu hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani umekamilika inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi fulani hivyo ameuagiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko nje ikoje.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.

Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top