Friday, 10 March 2017

Bulembo atangaza kujiuzulu nafasi yake ndani ya CCM.|Soma

Ikiwa ni siku nne tu zimepita tangu Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba kusema kuwa hana mpango tena wa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi ujao, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM naye amesema kuwa miaka mitano aliyotumikia nafsi hiyo inatosha, hivyo ni wakati wake kupumzika.

Alhaji Abdallah Bulembo alitangaza uamuzi huo wa kujiuzulu jana wakati akifungua kikao cha dharura cha jumuiya hiyo walipokuwa wakijadili mapendekezo yaliyotolewa na Halmahsauri Kuu wa CCM iliyokutana Disemba mwaka jana.

Bulembo aliwaambia wajumbe hao kuwa anajiuzulu na nafasi hiyo na kuwa sababu si kwa vile ameteuliwa kuwa mbunge bali yeye anaamini ni muda wa kupisha mtu mwingine.

Aidha, aliwataka viongozi hao kujipima kuona kama kuna ambaye anaona kuwa anaweza kuongoza jumuiya hiyo agombee.

Lakini aliwaasa wote watakaogombea kuwa, yeye hatompigia mtu kampeni na wala asiwepo mtu atakayesema kuwa amekubaliana naye jambo lolote, hivyo kila mgombea ajinadi mwenyewe.

Pia Bulembo alisema kwa muda wote ambao ameingoza jumuiya hiyo, amefanikiwa kwa asilimia 75 kwa yote aliyoyaahidi kwani wakati anaingia madarakani jumuiya hiyo ilikuwa katika hali mbaya hadi mwenyekiti aliyekuwepo, Dkt Kikwete akataka kuifuta.

"Tangu nimeingia madarakani hatujawahi kuomba hata shilingi mia kwa ajili ya kuendesha vikao vyetu, "alijisifu Bulembo.

Hata hivyo amesema ataendelea na majukumu ya nafasi hiyo hadi mwezi Oktoba atakapokabidhi ofisi kwa mwenyekiti mpya atakayechaguliwa.

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top