Thursday 16 February 2017

DUBAI: Abiria kuanza kubebwa kwa ndege zisizo na marubani huko Dubai.|Soma

Ndege itakayoanza kutumika Dubai

Ndege isiyokuwa na rubani ambayo inaweza kuwabeba watu, itaanza kutumiwa kwa uchukuzi wa abiria Dubai mwezi Julai, mkuu wa uchukuzi katika jiji hilo ametangaza.


Ndege hiyo muundo wa eHang 184 kutoka China tayari imefanyiwa majaribio, Matt al-Tayer amesema.


Ndege hiyo inaweza kubeba abria mmoja wa uzani wa kilo 100 na inaweza kupaa kwa dakika 30 kwa wakati mmoja.


Ndege hiyo ina skrini ya kompyuta ambapo mtu anaweza kubofya na kuchagua anataka kwenda wapi.


Hamna mitambo mingine yoyote ya kutumiwa na mtu kudhibiti ndege hiyo kutoka ndani.


Ndege hiyo inaweza kupaa kwa kasi ya maili 100 kwa saa (kilomita 160 kwa saa) na inaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 baada ya betri yake kujazwa chaji.

 

"Huu si mfano au ndege ya kufanyiwa majaribio," Bw al-Tayer alisema kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press.

 

"Tayari tumeufanyia majaribio mpango huu. Ndege hii imepaa katika anga la Dubai."


Ndege hiyo pia iliidhinishwa baada ya kufanyiwa majaribio Nevada nchini Marekani Juni 2016.


Mhadhiri wa ngazi ya juu wa masuala ya uchukuzi wa ndege katika Chuo Kikuu cha England Magharibi Dkt Steve Wright, ameambia BBC kwamba itakuwa muhimu kuzingatia usalama.

 

"Ni changamoto kuhakikisha kwamba mifumo inayotumiwa haiwezi kuacha kufanya kazi (abiria akiwa angani)," alisema.


Alidokeza kwamba angependa kuona kwamba ndege hiyo ikipaa kwa zaidi ya saa 1000 kwanza kabla ya binadamu kuingia ndani. Haki miliki ya picha AP Image caption Ndege hiyo ilifanyiwa majaribio Nevada mwaka 2016.


Dkt Wright amesema hawezi kuwa mmoja wa abiria wa kwanza.

 

"Itabidi wanaoniingiza ndani ya ndege kama hio watumie nguvu zaidi, na nitakuwa ninapigana na kupiga mayowe."


Mwezi uliopita, kampuni ya Israel ya Urban Aeronautics ilitangaza kwamba ndege yake isiyo na rubani - ambayo iliundwa kwa matumizi ya kijeshi - ingeanza kutumika kufikia 2020, lakini sana katika uokoaji.


Ndege hiyo ya thamani ya $14m (£11m) inaweza kubeba mzigo wa kilo 500 (1,100lb) kwa kasi ya 185km/h (115mph).


Chanzao: BBC

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top