Monday, 16 January 2017

Ndege ya Uturuki yaangukia nyumba Kyrgyzstan na kuua watu 32.|Soma

Ndege ikiwa imeangukia makazi ya watu karibu na mji wa Bishkek

Watu zaidi ya 32 wamefariki baada ya ndege ya kubeba mizigo ya Uturuki, iliyokuwa safarini kutoka Hong Kong, kuangukia nyumba za watu karibu na mji wa Bishkek nchini Kyrgyzstan.

 


Wengi wa walioangamia ni watu waliokuwa ardhini, maafisa wanasema.

 


Ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilianguka karibu na uwanja wa ndege wa Manas, takriban kilomita 25 kutoka mji mkuu Bishkek, serikali ya Kyrgyzstan imesema.

 


Nyumba zaidi ya 15 zimeharibiwa na watoto kadha wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waliofariki.

 


Ndege hiyo ilikuwa imepangiwa kutua kwa muda Manas na kisha kuendelea na safari hadi Istanbul, uturuki.

 


Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la ndege za kubeba mizigo la ACT, ambayo hujitambulisha kama MyCargo.

 


Hata hivyo, serikali ya Kyrgyzstan inasema ndege hiyo ilikuwa inasafiri chini ya shirika la ndege la serikali ya Uturuki,


Maafisa wa shirika hilo hata hivyo wamekanusha taarifa hizo kwenye Twitter.

 


"Ramirambi zetu kwa jamaa za waliofariki katika ajali hii mbaya iliyohusisha ndege ya shirika la ACT Airlines nchini Kyrgyzstan," Turkish Airlines wameandika. Haki miliki ya picha Reuters Image caption Kulikuwa na ukungu kutokana na baridi kali.

 

Chanzo: BBC

0 comments:

Copyright © 2017 KwilasaNewsline | We Call Away| All Right Reserved|
Scroll To Top