Wasichana wa Tanzania kujadiliana na Michelle Obama
Wasichana 25 wa Tanzania
wanatarajiwa kufanya majadiliano ya moja kwa moja na mke wa Rais wa
Marekani, Bi Michelle Obama wiki ijayo.
Wasichana hao ni miongoni
mwa wasichana wa nchi tatu watakaoshiriki majadiliano hayo yenye lengo
la kumuwezesha mtoto msichana katika masuala mbalimbali na upatikanaji
wa fursa na kuzungumuzia hali ya ukatili wa kijinsia nchini Tanzania. Nchi zingine ni Peru na Cambodia.
Majadiliano hayo ni tukio litakalofanywa na Shirika la
Plan International Tanzania na yatafanyikia katika ubalozi wa Marekani,
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Msichana Duniani tarehe 11 Oktoba,
2016.
0 comments:
Post a Comment