Mataifa yenye Wanafunzi Vichwa zaidi Duniani...Orodha hii hapa
Katika kutathmini viwango vya elimu
duniani, wengi wamekuwa wakiangazia sana ubora wa vyuo. Lakini kwa
jumla, ni mataifa gani yenye wanafunzi walio bora zaidi?
Jambo la kushangaza ni kwamba orodha hii inaonyesha taswira tofauti sana na ile inayotolewa na utathmini wa vyuo vikuu.
Shirika
la Kimataifa la Uchumi na Maendeleo (OECD) limefanya wazi matokeo ya
mtihani wa kupima uwezo wa wanafunzi wanaohitimu kutoka nchi mbalimbali.
Orodha ya ubora wa vyuo vikuu hutawaliwa na vyuo vikuu kutoka
Marekani na Uingereza kama vile Harvard, MIT, Stanford, Oxford,
Cambridge na UCL.
Lakini baada ya OECD kuchunguza uwezo wa kusoma
na kuandika miongoni mwa wahitimu kutoka vyuo vikuu, wanafunzi walio
bora zaidi ilibainika wanatoka Japan na Finland na wala si Marekani na
Uingereza..
Nchi zenye wanafunzi bora zaidi wanaohitimu kwa mujibu wa OECD
1.Japan
2. Finland
3. Uholanzi
4. Australia
5. Norway
6. Ubelgiji
7. New Zealand
8. England
9. Marekani
10. Jamhuri ya Czech
Nchi hizi zote huwa mara nyingi hazina chuo haka kimoja kinachokuwa kwenye orodha ya vyuo vikuu 10 bora duniani.
Badala ya vyuo vikuu vya Marekani kufana, yamkini vyuo vikuu vya Norway na Australia vina wanafunzi bora wanaohitimu.
Kwa mujibu wa orodha ya ubora wa vyuo ya QS World University Rankings, kulikuwa na vyuo 32 vya Marekani katika 100 bora, na chuo kikuu kimoja pekee kutoka New Zealand.
Lakini ripoti ya OECD inaonesha wanafunzi wa New Zealand wanafanya vyema kushinda wenzao Marekani.
0 comments:
Post a Comment