CUF ya pewa siku 14 kupinga maamuzi ya Msajili wa vyama vya Siasa.
Leo kupitia ukrasa wa facebook Julius Mtatiro kaandika haya kuhusiana na CUF;
"Mahakama kuu Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo tarehe 10/10/2016
imetoa ushindi kwa Chama cha Wananchi (CUF) kwa kutoa kibali cha
kisheria kwa chama kuwasilisha ndani ya siku 14, kesi ya kuiomba
mahakama kutengua maamuzi batili ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini,
kwani maamuzi hayo batili yametengua maamuzi halali ya vikao halali vya
chama.
Mawakili wa CUF wakiongozwa na Mhe. Juma Nassor, Mhe. Daimu na
Mhe. Hashim Mziray wamewaahidi wanachama wa CUF nchi nzima kwamba
wataifungua kesi husika ndani ya wiki hii. Kwa kawaida, uamuzi wa leo wa
Jaji Munisi huweza kufanywa upande mmoja (EXPARTE) kama ilivyofanyika".
0 comments:
Post a Comment